Friday, May 4, 2018
KILIMO BORA CHA ALIZETI
Alizeti au kifuata-jua au mkabilishamsi (Helianthus annuus) ni mmea unaodumu mwaka mmoja mwenye ua kubwa. Asili yake iko Amerika lakini imeenea pande nyingi za dunia.
Alizeti inafikia urefu hadi mita 3 na ua lake upana hadi 30 cm.
Kiasili alizeti inapatikana katika Amerika. Maindio walipanda ua katika bustani zao. Wahispania walileta mbegu Ulaya baada ya kufika Amerika na mwanzoni mme ulipandwa kama ua la mapambo kwenye bustani.
Baadaye kiwango kikubwa cha mafuta ndani ya mbegu zake kilitambuliwa kikawa mme muhimu cha kuzaa mafuta.
Kufuata juaEdit
Jua linapochomoza maua mengi ya alizeti hugeukia mashariki jua linapotokea, na wakati wa mchana huendelea kulifuata jua mpaka magharibi hurudi katika uelekeo wa mashariki tena. Mwendo huu, “heliotropism”, huratibiwa na seli ziitwazo ‘pulvinus’ sehemu iliyo huru kuzunguka chini kidogo tu ya chipukizi. Hatua ya chipukizi inapo isha shina hukomaa na mmea hupoteza uwezo wake wa kuzunguka tena kulifuata jua. Mmea huganda kuelekea ( mara nyingi) upande wa mashariki. Majani na shina hupoteza rangi yake ya kijani. Mimea ya pori jamii ya alizeti huwa haizunguki kufuata jua, japo majani yake hufuata jua maana yao huelekea upande wowote pindi yanapokomaa.
HistoriaEdit
head snack.jpg [1] Mmea huu una asili ya katikati ya Amerika. Wataalamu wamekadiria kuwa ulianza kulimwa sana huko Meksiko, mnamo mwaka 26000 KK na pia huko bonde la mto Mississippi. Mifano ya mimea iliyotolewa Meksiko imeonekana huko Tennessee, Marekani pia, ikionesha kuwa pale tangu 2300K.K.[2] Watu wengi wanatumia mmea wa alizeti kama ishara ya nguvu na utakatifu wa jua, hasa wale wa alizeti kama ishara ya nguvu na utakatifu wa jua. Hasa wale wa Aztecs na Otomi wa Meksiko na kusini mwa Amerika. Francisco Pizarro alikuwa mtu wa kwanza kutoka Ulaya kuuona mmea wa alizeti huko Peru. Taswira ya dhahabu ya mmea na mbegu zake zilichukuliwa na kupelekwa Hispania mnamo karne ya 16. Baadhi ya watafiti wanasema kuwa Hispania iliwekewa vikwazo vingi kilimo cha alizeti kutokana na imani ya dini imayoambatana na mmea huo. [3] Kufikia karne ya 18, matumizi ya mafuta ya alizeti yalikuwa maarufu mno, hasa kwa waumini wa kanisa la Russia la Orthodox kwa sababu mafuta ya alizeti yalikuwa miongoni mwa vitu vichache vilivyo kuwa vinaruhusiwa kutumika wakati wa kwaresma.
Kilimo na matumiziEdit
Kukua vizuri mmea wa alizeti unahitaji jua la kutosha. Hakuna vyema kwenye arthi iliyo na rutuba ndogo wenye ukame mzuri na matandazo ya kutosha katika kilimo cha bidhaa mbegu hupandwa kwa umbali was m 45 na kinaacha 2.5. mbegu yam mea huu, alizeti, huliwa kama chakula cha kutafuna baada ya kuokwa/ kukaushwa, pamoja au bila ya chumvi. Huko ujerumani hutumika kutengenezea mikate. Alizeti pia ni chakula cha ndege na hutumika kwenye mapishi moja kwa moja na wakati wa kuandaa saladi. Mafuta ya alizeti yanayokamuliwa kutoka kwenye mbegu za alizeti hutumika kupikia, mafuta ya kutunzia vitu na huzalisha siagi na dizeli ya mimea. Sababu yana gharama ndogo kuliko mafuta ya mizeituni. Kuna mimea mingi ya jamii ya alizeti yenye aina mbalimbali na viwango mbalimbali vya mafuta.mashudu yanayobaki baada ya kukamua mafuta hutumika kulishia mifugo kama chakula, alizeti pia huweza kuzalisha mpira.
Alizeti pia hutumika kufyonza kemikali hatari kutoka ardhini kama vile urani na walitumika katika kuondoa madini ya urani ardhini baada ya janga la kinyuklia lililotokea huko Chernobyl.
Contact/ Wasiliana nasi
Phone (Simu): +255766797400 Email: daudilyela@yahoo.com
Our Services ( Huduma zetu): Research( Utafiti), Project Proposal ( Mapendekezo ya Miradi), Business Plan ( Plani za Biashara), Profit Assessment ( Upimaji wa Faida),
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
KILIMO BORA CHA NDIZI
Ndizi ni tunda muhimu Afrika ya Mashariki na katika nchi za joto kwa jumla hasa visiwa vya caribian. Mmea wake huitwa mgomba. Kibiolojia n...
-
UTANGULIZI Tango ni zao linalopendelea hali ya hewa ya joto na husitawi vema kati ya nyuzi joto 18°C hadi 35°C Udongo Hustawi vizuri katika ...
-
UTANGULIZI Nyanya Chungu au Ngogwe ni zao la kitropic linalotoa mazao yake kama matunda na kutumika kama mboga, kuna aina mbalimbali za nya...
-
UTANGULIZI Tikiti maji ni tunda ambalo kisayansi hujulikana kama Citrullus lanatus katika familia ya Cucurbitaceae , ambalo mmea wake hutoa...
No comments:
Post a Comment