Friday, May 4, 2018
KILIMO BORA CHA TANGAWIZI
UTANGULIZI
Tangawizi ni aina ya zao la kiungo ambalo sehemu inayotumika ni tunguu ( rhizome) ambalo huonekana kama mizizi ya mmea. Kwa jina la kitalamu ni Zingiber officinale. Pia ni mmea wenye majani ya kijani na maua yake ni mekundu. Tangawizi inaota kutoka kwenye mzizi ulioota.
ASILI YAKE
Tangawizi asili yake ni maeneo ya bara la Asia,nchi kama China, Japan, and India, lakini sasa Tangawizi inamea maeneo kama Amerika kusini na Bara la Africa. Na kiasi flani inapandwa uarabuni na kutumika kama dawa na kutumika kama kiungo. Zao hili linazalishwa sana nchi ya Jamaica. Hapa nchini zao hili hulimwa sana katika mikoa ya Tanga, Mbeya, Kilimanjaro, Kigoma, Morogoro na Pwani.
FAIDA KIAFYA
Tangawizi kwa kawaida inatumika kutibu “matatizo mbalimbali ya tumbo” na magonjwa mengineyo, matatizo ya maumivu wakati wa asubuhi, gesi katika tumbo, kuharisha, kulia kwa watoto mara kwa mara, kichefuchefu, kichefuchefu kinachotokan ana matitabu ya kansa, kichefuchefu kinachotokana na matibabtu ya Upungufu wa kinga mwilini (UKIMWI), kichefuchefu na kutapika baada ya kufanyiwa upasuaji na ukosefu wa hamu ya kula.
Matumizi mengine yakihusishwa na maumivu kutokana na maumivu ya viungo, maumivu kutokana na hedhi, kikohozi, matatizo ya upumuaji, kichwa kuuma, mkamba na kisukari. mara nyingine Tangawizi inatumika kupunguza maumivu ya kifua, mgongo, na maumivu ya tumbo, anoreskia, kuchochea ongezeko la maziwa kwenye matiti, dawa ya kikojozi, na kuongeza utamu. inatumika pia kama kinga ya kipindupindu, kutokwa na damu, kuharisha damu, malaria, sumu kwa kuumwa na nyoka, maumivu kwenye meno.
Wengine hutumia kama kinga ya ngozi kwa kutengeneza juice kama mafuta. Mafuta yatengenezwayo mara nyingine hutumika kama kituliza maumivu na kuzuia wadudu kwenye ngozi.
Katika chakula na vinywaji Tangawizi hutumika kama kiongeza ladha
Katika uzalishaji (Viwandani) Tangawizi hutumika kama harufu katika sabuni na vipodozi.
MATUMIZI
Kichefuchefu na kutapika kutokanako na kutibu Upungufu wa kinga mwilini (UKIMWI). Utafiti unapendekeza kutumia Tangawizi kila siku, dakika 30 kabla kila dozi ya kupunguza makali kwa siku 14, inapunguza hatari ya kutapika na kichefuchefu kwa mgonjwa.
Maumivu kipindi cha hedhi. Utafiti unaonesha kuwa kupata mg 1500 ya Tangawizi mara tatu kwa dozi kila siku katika siku tatu za mwanzo za kipindi cha hedhi inasaidia kupunguza maumivu katika hedhi na dalili zake. Mafunzo mengine yanatuonesha kuwa kutumia Tangawizi maalum (Zintoma, Goldaru) mg 250 mara nne kila siku mwanzoni mwa kipindi cha hedhi pia inapunguza maumivu na dalili zaidi ya asilimia 62% ya watu. inasemekana hufanya kazi kama madawa mengine.
Ugonjwa unaotokea asubuhi. Kutumia Tangawizi mdomo inasemekana inapunguza kichefuchefu na kutapika kwa wajawazito. Lakini itafanya kazi taratibu au sio sawa na dawa zingine zinazotumika kutibu kichefuchefu. Pia kutumia dawa zingine ni uamuzi mzuri. Kabla hujatumia Tangawizi.
Osteoarthritis. Baadhi ya tafiti zinaonesha kuwa kutumia Tangawizi inapunguza maumivu kwa watu wenye fomu ya jongo unaoitwa “osteoarthritis.” Mafunzo yanaonesha kutumia mg 250 ya Tangawizi maalum (Zintona EC) mara nne kwa siku inapunguza maumivu ya jongo katika goti baada ya matibabu ya miezi mitatu. Mafunzo mengine yanaonesha kuwa kutumia aina mbalimbali za Tangawizi (Eurovita Extract 77; EV ext-77), ambazo zinaunganisha Tangawizi na alpinia, pia inapunguza maumivu yanayotokea wakati wa kusimama, kutembea na ugumu. Baadhi ya tafiti zilizolinganisha Tangawizi na dawa mengine kama ibuprofen. Moja ya mafunzo, kwa aina ya Tangawizi (Eurovita Extract 33; EV ext-33), kutumia mg 500 ya Tangawizi mara mbili kila siku ni sawa na kutumia dawa mg 400 ya ibuprofen mara tatu kila siku kwa maumivu ya hip na goti pamoja na arthritis. Katika mafunzo mengine, Tangawizi maalum iliyochanganywa na glucosamine (Zinaxin glucosamine, EV ext-35) inafanya kazi kama dawa mpinga uchochezi wa magonjwa (mg 100 kila siku) jumlisha glucosamine sulfate (gram 1 kila siku). Tafiti pia zinashauri kuwa kufanya massagi kwa mafuta yenye Tangawizi na Chungwa inapunguza ugumu na maumivu kwenye goti.
Kichefuchefu na kutapika kutokana na upasuaji. Utafiti wa kiafya unaonesha kwamba kutumia gramu 1 hadi 1.5 ya Tangawizi saa moja kabla ya upasuaji itapunguza kichefuchefu na kutapika kati ya masaa 24 baada ya upasuaji. Kuna fundisho lilipatikana kuwa Tangawizi inapunguza kichefuchefu na kutapika kwa asilimia 38%. Pia, kumpaka mgongwa mafuta ya Tangawizi maeneo anayofanyiwa upasuaji kabla ya upasuaji yamesaidia kuzuia kichefuchefu kwa wagongwa asilimia 80%. Japo, ikitumiwa kwa kunywa inaweza isipunguze kichefuchefu na kutapika ndani ya masaa 3-6 baada ya upasuaji. Pia, Tangawizi haiwezi kuwa na athari/ matokeo pale unapotumia dawa zingine za kichefuchefu na kutapika. Kwa nyongeza, .
Kizunguzungu. Kutumia Tangawizi inapunguza dalili za kizunguzungu, kikiambatana na kichefuchefu.
KILIMO CHA TANGAWIZI
HALI YA HEWA NA UDONGO
Zao hili hustawi katika maeneo yenye hali ya kitropiki, kutoka usawa wa bahari hadi mwinuko wa mita 1,500 au zaidi. Huhitaji mvua kiasi cha mm.1,200-1,800 na joto la wastani wa nyuzi za sentigredi 20-25. Hustawi vema katika udongo tifutifu wenye rutuba na usiotuamisha maji.
UTAYALISHAJI WA SHAMBA
Kuandaa shamba Tangawizi unaweza kutumia trecta, jembe la mkono au la ng’ombe kutayarisha shamba, shamba litayarishwe mwezi mmoja kabla ya kupandikiza kwa kukatua ardhi hadi kufikia kina cha sentimita 30. Lainisha udongo. Shamba linatakiwa kuandaliwa vituta vidogo vidogo kwa nafasi ya sentimita 75 kutoka tuta hadi tuta, hiihusaidia kuhifadhi udongo na maji na hutoa nafasi nzuri wakati wa upanukaji wa viazi. Inashauriwa pia kama matuta hayajatumika basi ni muhimu kujaza udongo kwenye shina kwani pingili za chini kwenye shina ni lazima zifunikwe na udongo ili zitoe viazi kwa wingi na hivyo mavuno huongezeka.
UTAYALISHAJI WA MBEGU
Mbegu iandaliwe mapema mwezi mmoja kabla ya kupanda na pia itunzwe katika mazingira mazuri kwenye kivuli pasipo na jua ikiwezekana weka ndani ya chumba kinachopitisha hewa, pindi unapokwenda kupanda katakata vipande urefu wa nchi moja na hakikisha tunguu haijakauka. Kiasi cha kilo 840-1700 cha vipande vya tunguu huweza kutumika kwa kupanda katika hekta moja.
UPANDAJI
Zao la tangawizi hupandwa kwa kutumia vipande vya tunguu vyenye kichipukizi kizuri angalau kimoja na huweza kukatwa katika urefu wa sm.2.5-5. Tangawizi humea na kukomaa baada ya miezi 8 mpaka 10. Wakati mwingine, vichipukizi vinavyopatikana katika kumenya tangawizi huweza kuhifadhiwa na kutumika kwa kupanda. Kiasi cha kilo 840-1700 cha vipande vya tunguu huweza kutumika kwa kupanda katika hekta moja. Nafasi inayotumika kupanda ni kati ya sentimita. 23-30 kwa 15-23 na kina cha sentimita.5-10 na mara nyingi hupandwa katika matuta. Baadhi ya mazao huweza kupandwa katika shamba la tangawizi ili kuweka kivuli chepesi ingawa si lazima kivuli kiwepo. Inashauriwa kumwagilia maji endapo mvua inakosekana. Na inahitaji uangalizi kwa matokeo bora.
MBOLEA
Weka mbolea za asili zilizooza vizuri kiasi cha ndoo moja hadi mbili, kwa eneo la mita mraba 10. Mbolea hii iwekwe katika kila shimo. Kiasi kinachotakiwa ni kilo moja au kopo moja la Tanbond kwa kila shimo. Hii ni sawa kuweka na tani 10 hadi 20 kwa hekta. Baada ya wiki 1-2 kabla ya kupanda weka mbolea ya samadi au mboji kiasi cha tani 25-30 kwa hekta na kwa kukuzia weka kiasi cha NPK kwa uwiano wa kilo 36:36:80. Tandaza nyasi shambani kuhifadhi unyevunyevu hasa pale kivuli kinapokosekana.
UPALILIAJI
Palizi hufanywa mara magugu yanapoota, dawa ya kuua magugu, kama simazine hutumika. pandishia tuta ili kufanya tangawizi kutunza unyevu na huota vizuri
Tangawizi iliostaawi vizuriTangawizi iliyotayari kwa kupandwa (Mbegu)
MAGONJWA NA WADUDU
• Madoa ya majani yanayosababishwa na viini vya magonjwa viitwavyo Colletotrichum zingiberis na Phyllosticta zingiberi.
• Kuoza kwa tunguu; kunasababishwa na viini viitwavyo Pithium spp • Mizizi fundo; inasababishwa na Meloidegyne spp.
UVUNAJI
Tangawizi huweza kuwa tayari kwa kuvuna kati ya miezi 9-10 baada ya kupanda, wakati majani yake yanapogeuka rangi kuwa njano na mashina kusinyaa. Tangawizi inayohitajika kwa kuhifadhi kwenye kemikali (preserved ginger in brine) huvunwa kabla haijakomaa kabisa, wakati ile iliyokomaa kabisa huwa kali zaidi na huwa na nyuzi hivyo hufaa kwa kukausha na kusaga. Mavuno hutofautiana kulinganana na huduma ya zao, mavuno yanaweza kuwa kiasi cha tani 20-30 cha tangawizi mbichi huweza kupatikana.
USINDIKAJI
Tangawizi ikisindikwa utapata unga, mafuta maalum (essential oils) n.k. Tangawizi iliyovunwa huweza kumenywa, kukatwa na kukaushwa juani au mara nyingine huchovywa katika maji yaliyochemka kwanza na ndipo kukaushwa au hukamuliwa mafuta. Pia tangawizi husindikwa na kuhifadhiwa kwenye chupa zikiwa zimechanganywa na sukari na/au chumvi. Hata hivyo tangawizi ina Kiasi cha mafuta cha 16.0-18.0%.
SOKO LA TANGAWIZI
Soko la tangawizi lipo ndani na nje ya nchi, kiasi kikubwa kinauzwa nchini. Bei yake ni kati sh. 300-1,500/- kutegemeana na msimu.
GHARAMA ZA UZALISHAJI NA MAPATO GHARAMA YA HEKTA MOJA:
Mbegu Tshs. 900,000/- Vibarua 250,000/- Mbolea(mboji/samadi) 150,000/- Jumla 1,300,000/-
MAPATO: Kilo 20,000 X300 =6,000,000/-
Contact/ Wasiliana nasi
Phone (Simu): +255766797400 Email: daudilyela@yahoo.com
Our Services ( Huduma zetu): Research( Utafiti), Project Proposal ( Mapendekezo ya Miradi), Business Plan ( Plani za Biashara), Profit Assessment ( Upimaji wa Faida),
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
KILIMO BORA CHA NDIZI
Ndizi ni tunda muhimu Afrika ya Mashariki na katika nchi za joto kwa jumla hasa visiwa vya caribian. Mmea wake huitwa mgomba. Kibiolojia n...
-
UTANGULIZI Tango ni zao linalopendelea hali ya hewa ya joto na husitawi vema kati ya nyuzi joto 18°C hadi 35°C Udongo Hustawi vizuri katika ...
-
UTANGULIZI Nyanya Chungu au Ngogwe ni zao la kitropic linalotoa mazao yake kama matunda na kutumika kama mboga, kuna aina mbalimbali za nya...
-
UTANGULIZI Tikiti maji ni tunda ambalo kisayansi hujulikana kama Citrullus lanatus katika familia ya Cucurbitaceae , ambalo mmea wake hutoa...
No comments:
Post a Comment