Friday, May 4, 2018
KILIMO BORA CHA UFUTA
UTANGULIZI
Ufuta (simsim/sesame) ni zao la kibiashara ambalo linatumika hasa kwa kuzalishia mafuta maana mbegu zake zina kiasi kikubwa cha mafuta kiasi cha asilimia 45 hadi 55.Na zao hili linaweza kulimwa maeneo mengi ya Afrika mashariki. Maeneo mbalimbali hutegemea zao hili kama la kibiashara maana linatoa kiasi kikubwa cha mafuta.
ASILI YAKE
Asili ya Ufuta ni Asia na Afrika. Ilikuwa ikilimwa sana nchini India, pia hata nchi ya China, Sudan, Uganda, Egypt, Mexico, Japan, Persia, Syria, Turkey, Greece.
HALI YA HEWA & UDONGO
Zao hili linawezwa kulimwa katika maeneo yanayopata mvua kidogo.Maeneo ya ukanda wa chini usawa wa bahari hufaa zaidi kwa kilimo cha ufuta.Pia nyanda za juu ambazo ni chini ya mita 1500 hufaa kwa kilimo cha ufuta.Mfano kwa Tanzania unaweza Ukalima ufuta katika mikoa ya Morogoro,Lindi,Manyara,Dodoma,Iringa. Ufuta ustawi vizuri katika maeneo yenye udongo mwepesi mweusi na usiotuamisha maji,udongo tifutifu ni mzuri kwa kilimo cha ufuta,Pia ufuta unawezwa kulimwa katika udongo wowote lakini usiotuamisha maji.Ufuta hufa haraka kama maji yatatuama kwa muda mrefu shambani.
UTAYALISHAJI WA SHAMBA
Shamba la Ufuta linatakiwa kutayarisha baada ya mavuno ya msimu uliopita, wiki mbili au wiki tatu kabla ya kupanda, hakikisha shamba lako lina udongo wenye rutuba na hautuamishi maji, kama shamba halina rutuba weka mbolea za asili (samadi au mboji).
UTAYALISHAJI WA MBEGU
Kuna aina kuu mbili za mbegu za ufuta:
1) MBEGU ZA ASILI
Wakulima wengi hupanda mbegu za asili, mbegu ambazo zilianza kulimwa miaka mingi iliyopita.Mbegu hizi nyingi zina mavuno kidogo na huchukua muda mrefu kukomaa Huchukua siku 140 hadi 180.
2) MBEGU ZA KISASA
Mbegu hizi zinakomaa kwa muda mfupi na hutowa mavuno mengi, wastani wa kilogram 500 hadi 800 kwa ekari kama shamba litaandaliwa litapandwa na litatunzwa vizuri.Mbegu hizi huchukua siku 105 hadi 140 kukomaa.Mfano wa mbegu hizi ni Naliendele 92,Lindi 202,Ziada 94 na Mtwara 2009.
UPANDAJI
Maandalizi bora yanaongeza uzalishaji, baada ya kuandaa shamba na kuandaa mbegu ndipo unaweza kupanda Ufuta.Inashauriwa kupanda ufuta kwa mistari kwa vipimo vifuatavyo.Sentimeta 50 kwa 10 au 50 kwa 20 kama utapanda kwa kutumia mistari ya kuchimba vijifereji vidogo katika mstari na kudondosha mbegu hizo katika vifereji hivyo (Drilling method) na kwa kuacha mche mmoja mmoja kwa kila shina.
Pia sentimeta 50 kwa 30 au 60 kwa 30 kwa kuacha miwili kwa kila shina. Kwa Mbegu ya Asili Unaweza Kupanda kwa sentimeta 70 kwa 30 kwa Kuacha Miwili kwa Kila shimo.Fukia mbegu kwa sentimenta .2.5 hadi 5. Muda mzuri wa kupanda ufuta ni mwanzoni mwa msimu wa kilimo yaani Mwishoni mwa mwezi Desemba hadi katikati kwa mwezi Januari.
MBOLEA
Ni bahati nzuri kuwa Ufuta hautumii mbolea nyingi. Tumia mbolea za asili kwa matokeo mazuri. Japokuwa hustawi zaidi katika udongo wenye rutuba ya kutosha.Kama utapanda katika ardhi isiyo na rutuba ya kutosha basi unaweza kutumia mbolea kiasi kidogo Mbolea kama vile UREA na BUSTA.
UPALILIAJI
Miche ya ufuta ni midogo na laini sana hivyo inahitaji palizi mapema hasa katika kipindi cha mwanzo wiki nne au tano .Pia katika kipindi hiki unatakiwa kupunguza miche iliyosongamana.Kadri utavyochelewesha palizi na kupunguzia mimea mapema ndivyo unavyoifanya mimea isikuwe vizuri na kujipunguzia kipato chako.
MAGONJWA & WADUDU
MAGONJWA
Ufuta hauna magonjwa mengi ila magonjwa yake makuu ni madoa ya majani na kuoza matawi na shina. Zuia magonjwa haya kwa Kupanda mbegu bora na kwa kutokupanda ufuta katika ardhi inayotuamisha maji,pia itawezekana kubadilisha shamba usilime ufuta katika shamba lililolimwa msimu uliopita.
WADUDU
Shamba la Ufuta kuna wadudu wengi wanaoshambulia ufuta kama vile vibaruti (Ambao hushambulia hatua ya mwanzo kabisa ya miche iliyoota ya ufuta ambapo vibaruti hula majani ya mwanzo ya mmea mara tu yanapojitokeza).Pia Aphidi hushambulia ufuta kwa kufyonza maji katika majani ya mimea hivyo kupelekea kukauka kwa majani ya mmea.
Pia wapo funza wa majani ambao hula majani ya mimea na pia hufunga majani ya ncha ya mimea na kuzuia ukuaji wa matawi wa mimea,wadudu hawa ni hatari zaidi kwani wanazuia kutengenezwa kwa vitumba vya ufuta.
Kuzuia Vibaruti
kabla hujapanda mbegu yako changanya na dawa ya tunza au gaucho.Pia panda mbegu bora na fanya mzunguko mazao shambani.Wadudu wengine wakijitokeza tumia dawa kama karate,dimethoate.Twigathoate,duduall,duduba na dawa nyingine za wadudu kabla wadudu hawajasababisha madhara makubwa shambani.
UVUNAJI
Dalili za ufuta kukomaa na kuwa tayari kwa kuvunwa ni pale ambapo utaonesha mabadiliko ya majani yake na shina na matawi yatabadilika rangi yake na kuwa njano au kahawia au yataanza kukauka,pia vitumba vya mwanzo vitaanza kubadilika rangi yake na kuanza kukauka hivyo utatakiwa ukate ufuta mapema kabla vitumba havijakauka na kupasuka.Vuna ufuta wako kwa kukata matawi ya ufuta na kuyafunga katika matita ya saizi inayokufaa ila yasiwe matita makubwa sana ambayo hayatakauka katikati kwa urahisi yasimamishe matita yako kuelekeza juu kisha acha yakauke kwa wiki mbili hadi nne kutegemea na ukali wa jua.vitumba vikisha kauka na kupasuka tandika mkeka au turubai na yageuze matita yako katika mkeka na turubai hapo ufuta utamwagikia katika mkeka au turubai lako,kuupata ufuta unaokwama katika matita piga piga kidogo tita
Contact/ Wasiliana nasi
Phone (Simu): +255766797400 Email: daudilyela@yahoo.com
Our Services ( Huduma zetu): Research( Utafiti), Project Proposal ( Mapendekezo ya Miradi), Business Plan ( Plani za Biashara), Profit Assessment ( Upimaji wa Faida),
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
KILIMO BORA CHA NDIZI
Ndizi ni tunda muhimu Afrika ya Mashariki na katika nchi za joto kwa jumla hasa visiwa vya caribian. Mmea wake huitwa mgomba. Kibiolojia n...
-
UTANGULIZI Tango ni zao linalopendelea hali ya hewa ya joto na husitawi vema kati ya nyuzi joto 18°C hadi 35°C Udongo Hustawi vizuri katika ...
-
UTANGULIZI Nyanya Chungu au Ngogwe ni zao la kitropic linalotoa mazao yake kama matunda na kutumika kama mboga, kuna aina mbalimbali za nya...
-
UTANGULIZI Tikiti maji ni tunda ambalo kisayansi hujulikana kama Citrullus lanatus katika familia ya Cucurbitaceae , ambalo mmea wake hutoa...
No comments:
Post a Comment