Friday, May 4, 2018

KILIMO BORA CHA BAMIA



UTANGULIZI
Bamia ni zao la mbogamboga linalolimwa sana sehemu za joto, kwa lugha ya kigeni inaitwa Okra. Zao hili hutumika kama mboga inayoliwa matunda yanayotokana na mmea. Zao hili linafaida sana kiafya, baadhi ya watu hutumia bamia kutengenezea mrenda. Aina za bamia zinazojulikana zaidi ni Clemson Spineless, Emerald Green, White Velvet, Perkins Mammoth na Dwarf Prolific.

ASILI YAKE
Asili ya mboga hii ni Afrika ya Kati na ya Mashariki, lakini kwa sasa zao hili limeenea katika sehemu nyingi za kitropiki, kama Visiwa vya Caribbean, Malaysia na Philipines. Zao hili kwa sasa hulimwa maeneo mengi.

HALI YA HEWA
Zao hili hustawi katika mete 1000 kutoka usawa wa bahari na hushindwa kuvumilia hali ya baridi kali. Hustawi katika katika aina nyingi za udongo na huhitaji mvua za wastani. Mimea yake haitumii chakula kingi kutoka ardhini. Iwapo ardhi haina rutuba ya kutosha inapendekezwa kuweka mbolea ya takataka au samadi.

UTAYALISHAJI WA SHAMBA
Lima shamba lako vizuri kwa kutumia trekta, jembe la ng’ombe, jembe la mkono au pawatila, hakikisha shamba linakuwa halina nyasi, changanya samadi au mboji na udongo ili kuongeza rutuba.

UTAYALISHAJI WA MBEGU
Andaa mbegu mapema kwa kawaida inapendekezwa kwanza kuweka mbegu katika chombo chenye maji ya vuguvugu kwa muda wa saa 24.Iwapo unyevu wa ardhi hautoshi, inapendekezwa kutumia mojawapo ya njia za kumwagilia maji kwenye bustani.

UPANDAJI
Mbegu za bamia hupandwa moja kwa moja katika bustani au shamba, lakini pia kwanza zinaweza kupandwa kwenye kitalu na kuhamishwa baadaye. Mbegu zimiminwe kidogo kidogo na miche ifikiapo urefu wa sentimeta 10 hadi 15, idadi yake ipunguzwe. Umbali wa unaopendekezwa ni sentimeta 40-50 kati ya mimea na sentimeta 70-80 kati ya mistari. Kilo moja hadi moja na nusu ya mbegu hutosha robo hekta ya bustani (zaidi ya nusu eka hivi).Aidha kuotesha ili kurahisisha uotaji mbegu mbili zipandwe kwenye shimo moja.
nafasi ya upandaji iwe ni sentimita 30 toka shimo hadi shimo na sentimita 50 toka mstari hadi mstari. Kwa zile aina zinazorefuka sana iwe sentimita 40 kati ya shimo na shimo na sentimeta 70 kati ya mstari na mstari.

MBOLEA
Katika zao hili inashauriwa kutumia mbolea za asili (samadi na mboji) au takataka ili kurutubisha ardhi na kupata mavuno mengi.

UPALILIAJI & UNYEVU
Shamba la bamia inatakiwa lipaliliwe kwa kuondoa nyasi na liwe safi ili kudhibiti magonjwa na wadudu, unyevu unahitajika ili kuongeza mavuno.

MAGONJWA &WADUDU

MAGONJWA
Zao la bamia pia hushambuliwa sana na ukungu uitwao ubwiri unga, pia hushambuliwa sana na utitiri mwekundu na aphids. Kwa hiyo kila wiki dawa ya ukungu na sumu ya wadudu ipuliziwe kwenye mimea ili kuweza kukua katika ustawi uliobora zaidi, pia ni vyema kuzuia kwa kufuata mzunguko wa mazao na kutumia dawa kulingana na ushauri wa wataalamu wa kilimo.

WADUDU
Mosaic Virus– Huu ni ugonjwa mbaya sana, majani huwa na madoamadoa na huumbuka. Haki hii hupunguza mazao. Nyunyizia dawa za sumu kuua wadudu.

UVUNAJI
•Bamia huvunwa kabla ya kukomaa yaani zikiwa bado changa.
•Kiasi cha kilo 8000 zaweza kupatikana katika ekari moja iwapo zitatunzwa vizuri.
•Hakikisha unavuna bamia na kikonyo chake, kisu kinaweza kutumika kwa kuvuna.

SOKO
Nchini Tanzania soko la bamia lipo. Inakadiriwa kuwa ifikapo kipindi cha masika bei ya bamia sokoni huwa juu. Hivyo mkulima atakayekuwa na mavuno ya bamia wakati wa masika anatarajiwa kuuza kwa bei ya juu kwa kuwa kipindi hicho zao hili huwa adimu katika soko.Ukilima eneo lenye ukubwa wa ekari 3 faida yake huwa kubwa zaidi kwani debe kidogoo cha lita 10 huwa 5000-6000 fedha za kitanzania.Ukilima kipindi cha kiangazi ambapo zao hilo huwa jingi sokoni hukadiriwa kidoo cha lita 20 huuzwa 3000-4000 fedha za kitanzania.
Contact/ Wasiliana nasi
Phone (Simu): +255766797400 Email: daudilyela@yahoo.com

Our Services ( Huduma zetu): Research( Utafiti), Project Proposal ( Mapendekezo ya Miradi), Business Plan ( Plani za Biashara), Profit Assessment ( Upimaji wa Faida),

No comments:

Post a Comment

KILIMO BORA CHA NDIZI

Ndizi ni tunda muhimu Afrika ya Mashariki na katika nchi za joto kwa jumla hasa visiwa vya caribian. Mmea wake huitwa mgomba. Kibiolojia n...