Friday, May 4, 2018
KILIMO BORA CHA MATUFAA – APPLES
KILIMO BORA CHA MATUFAA – APPLES
Tufaa ni tunda moja maarufu duniani ambalo hupendwa kuliwa na watu wa jamii zote, hii inatokana na utamu wake pamoja na faida za kiafya zinazopatikana kwa kula matufaa. Matunda haya hustawi zaidi kwenye nyanda za juu ambako joto sio kali, sehemu kama lushoto, Arusha, miteremko ya Kilimanjaro, Mbeya, Iringa, Njombe, Songea nk. Udongo ni wenye rutuba ya kutosha na usiotuamisha maji
Unaweza kupanda kwa kutumia mbegu au kwa kununua miche bora kutoka kwenye taasisiza kilimo mfano Uyole Mbeya. kama utatumia mbegu basi ni bora kununua mbegu bora au ukikosa mbegu basi jaribu kutumia zile utakazopata kutoka kwenye tunda lenyewe
Kama utachukua za kwenye tunda basi zikaushe kwenye jua kwanza mpaka zikauke kabisa, zile za kukununua huwa zimekauka kwa hiyo huna haja ya kuzikausha, Chukua karatasi laini (napkins/tissues) iloweshe maji kiasi kidogo kisha chukua mbegu zako na uzifunge na karatasi hii vizuri kisha ziwekw kwenye jokofu kwa kiasi cha wiki 3-4 zitaanza kuota/kumea, kuziweka kwenye friji husaidia kuua vijidudu vya magonjwa ambavyo huenda vilikuwepo kwenye tunda au mbegu
Chukua mbegu yako na uipande kwenye mifuko au chombo kama ndoo, usipande kwenye vifuko vidogo maana mmea huu hukua mkubwa kiasi na wenye mizizi mikubwa kabla ya kupandwa. Mmea wako ukifikia ukubwa wa futi moja mpaka pili ni kipindi kizuri kuuhamishia shambani,
Umbali wa shimo hadi shimo ni kiasi cha futi 15 mpaka 18 kutoka mti hadi mti. Hakikisha unapanda miche yako wakati wa mvua za kwanza, Mashimo yawe na kina cha futi mbili na upana futi 3. Weka kasi cha debe 1 la samadi au mboji na changanya vizuri na udongo.
kumbuka kuacha kisahani kwa ajili ya kukusanya maji ya mvua au unapomwagilia na utandaze majani/nyasi kiasi cha futi 3 kuzunguka mti wako, hakikisha wanyama kama mbuzi na ng’ombe hawaingii shambani na kula miti yako. Baada ya mwaka hutakuwa tena na haja ya kumwagilia miti yako kwani itaweza kukua yenyewe kwa kutegemea mvua
WADUDU NA MAGONJWA
Wadudu wanaoshambulia zaidi mitufaa ni vidukari (moth) na pia ugonjwa wa madoa meusi (black spot) ndio unaoshambulia zaidi, ili kupambana na ugonjwa na wadudu hawa hakikisha unatuma kiutilifu chochote che nye pareto (pyrethrum) ndani yake
KUVUNA
Uvunaji ni baada ya miaka mitatu lakini miche ya kuunga huanza kuzaa mapema hata ndani ya mwaka, ila nashauri usiruhusu matunda mengi kwenye miti midogo ili kuzuia matawi kuvunjika kwa hiyo punguza matunda kabla hayajawa makubwa na kubakisha machache
Contact/ Wasiliana nasi
Phone (Simu): +255766797400 Email: daudilyela@yahoo.com
Our Services ( Huduma zetu): Research( Utafiti), Project Proposal ( Mapendekezo ya Miradi), Business Plan ( Plani za Biashara), Profit Assessment ( Upimaji wa Faida),
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
KILIMO BORA CHA NDIZI
Ndizi ni tunda muhimu Afrika ya Mashariki na katika nchi za joto kwa jumla hasa visiwa vya caribian. Mmea wake huitwa mgomba. Kibiolojia n...
-
UTANGULIZI Tango ni zao linalopendelea hali ya hewa ya joto na husitawi vema kati ya nyuzi joto 18°C hadi 35°C Udongo Hustawi vizuri katika ...
-
UTANGULIZI Nyanya Chungu au Ngogwe ni zao la kitropic linalotoa mazao yake kama matunda na kutumika kama mboga, kuna aina mbalimbali za nya...
-
UTANGULIZI Tikiti maji ni tunda ambalo kisayansi hujulikana kama Citrullus lanatus katika familia ya Cucurbitaceae , ambalo mmea wake hutoa...
No comments:
Post a Comment