Friday, May 4, 2018

KILIMO BORA CHA ILIKI



UTANGULIZI
Iliki ni moja kati ya mazao ambayo yanatumika sana karibia kila siku kwenye matumizi ya nyumbani,utumika kama viungo kwenye chakula na pia utumika kama tiba ya magonjwa mbalimbali.na pia ni mmea mfupi ambao unatoa matunda kwa miaka mingi.

AINA ZA ILIKI
Kuna aina mbili za iliki ambazo ni



malabar-huzaa kwa kutambaa ardhini na matunda yake ni madogo madogo.urefu wa mmea wa malabar ni karibia mita 3
mysore-matunda yake huzaliwa kwa wima,majani mapana na mmea una urefu zaidi ya mita3

MAZINGIRA NA HALI YA HEWA

Huoteshwa kwenye maeneo yenye mvua 2500mm kwa mwaka
kivuli cha wastani
udongo wenye rutuba ya kutosha na ulio na unyevunyevu wa kutosha

KUPANDA
kunanjia mbili za kuotesha iliki unaweza kupanda mbegu au ukapanda miche midogo(spilits)
sia mbegu kwenye kitalu pandikiza mche shambani zikiwa na umri wa miezi 3-4 au zaidizenye ukubwa wa sm 15 au zaidi au tenganisha vimiche vinavyo zaliwa kwenye tunguu moja chini ya ardhi na pandikiza shambani.
tengeneza mashimo sm 60 x 60 na nafasi ya shimo panda miche kwenye mashimo.

KUTUNZA
Weka matandazo
ondoa mashina ya zamani na yalio nyauka
rekebisha kivuli

WADUDU NA MAGONJWA

Zuia wadudu waalibifu na magonjwa ili kupata mavuno mengi nayenye ubora
kuoza kwa majani-dhibiti kwa kupiga dawa zenye morututu k.m dithane m-45
virus(mosaic virus)- dhibiti kwa kutumia aina inayo vumilia
inzi mafuta zuia kwa kutumia dawa za kuuwa wadudu insecticides

KUVUNA
Huchukua miaka 3 tangia kupandwa mpaka kuzaa na kuvuna pale unapopanda miche midogo
ukipanda mbegu huchukua miaka 4-5 mpaka kuvuna
matunda huvunwa hasa mwezi march na april
matundwa huvunwa na kukaushwa kwenye jua

na kipanda kunauwezekana wa kuvuna 112-300 kwa heka na 45-120kg kwa eka ikiwa imekaushwa
Contact/ Wasiliana nasi
Phone (Simu): +255766797400 Email: daudilyela@yahoo.com

Our Services ( Huduma zetu): Research( Utafiti), Project Proposal ( Mapendekezo ya Miradi), Business Plan ( Plani za Biashara), Profit Assessment ( Upimaji wa Faida),

No comments:

Post a Comment

KILIMO BORA CHA NDIZI

Ndizi ni tunda muhimu Afrika ya Mashariki na katika nchi za joto kwa jumla hasa visiwa vya caribian. Mmea wake huitwa mgomba. Kibiolojia n...